Home » Uchunguzi Wa Mauaji Ya Jeff Mwathi Unakaribia Kwisha

Maafisa wa upelelezi kutoka Idara ya Upelelezi na makosa ya jinai DCI wamedokeza kuwa wanakaribia mwisho wa uchunguzi wa wiki tatu kuhusu kifo cha kutatanisha cha marehemu Geoffrey ‘Jeff’ Mwathi.

 

Kulingana na DCI, Mwathi, 23, aliuawa kabla ya kutupwa nje ya dirisha la ghorofa ya 10 la nyumba ya msanii wa Mugithi Lawrence Njuguna almaarufu DJ Fatxo katika Apartments za Redwood huko Kasarani mnamo Februari 22, 2023.

 

Kifo hicho ambacho kilizua taharuki kwa umma, kilisababisha DCI kufanya uchunguzi kufuatia ombi la mkuu wa idara, Amin Mohammed.

 

Katika taarifa leo hii Alhamisi, DCI imesema kwamba sampuli za DNA zimepatikana kutoka kwa marehemu ili kubaini kama madai ya unyanyasaji wa kingono kabla ya kifo cha marehemu yana mashiko.

 

Kufikia sasa, wapelelezi wamefanya uchunguzi wa mwili wa maiti kutoka sehemu za siri za nyuma, miongoni mwa sampuli nyingine, zilichukuliwa na kufanyiwa vipimo vya DNA ili kubaini ikiwa Mwathi alilawiti au la.

 

Hii ilikuwa baada ya wataalam wa uhalifu kuzuru tena (nyumba ya DJ Fatxo) mnamo Machi 29 na kufanya urekebishaji wa eneo la kisayansi na kurekodi taarifa mpya kutoka kwa mashahidi katika nia ya kutegua fumbo la kifo.

 

DJ Fatxo amekana kuhusishwa na kifo hicho, akisema kuwa yuko tayari kufanya kazi na wapelelezi kufichua ukweli kuhusu suala hilo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!