UDA Yamshutumu Raila Kuhusu Masharti Aliyotoa
Chama cha (UDA) kimetaja masharti yaliyowekwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa mazungumzo na serikali kuwa hayana mashiko.
Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Cleophas Malala Jumanne, UDA imepuuzilia mbali matakwa ya Azimio ikisema kuwa chama kinachoongozwa na Rais Ruto hakitatishika kuangukia kwenye njia za mazungumzo kinyume na katiba.
Kulingana na Malala, madai ya Odinga yanatolewa kulazimisha serikali kugawana mamlaka na Azimio.
Malala amekariri kwamba wito wa hivi majuzi wa rais wa mazungumzo na kiongozi wa Azimio haupaswi kukosolewa kama ishara ya uoga.
Matamshi ya Malala yanajiri baada ya Odinga kusema Azimio inataka kufanya mazungumzo katika ngazi ya kitaifa sawa na ile ya 2008 ambayo iliongozwa na Koffi Anan wakati wa marehemu Rais Mwai Kibaki.
Rais Ruto pia amesisitiza kuwa hakutakuwa na handsheki kati yake na kiongozi huyo wa Azimio….amezungumza hayo akiwa Kigali Rwanda kwa shughuli ya kiserikali.