Home » Trump Kufikishwa Mahakamani

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameelekea New-York, akitokea jimbo la Florida ambako ameratibiwa  kufika mahakamani kuhusiana na tuhuma na  kashfa ya kumlipa pesa mcheza filamu za ngono kabla ya uchaguzi wa mwaka 2016.

 

 

Hali ya usalama imeimarishwa vilivyo  katika eneo la Manhattan, mahali ambako mahakama atakayewasilishwa Trump inapatikana. Trump ni rais wa zamani wa Marekani wa kwanza  kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu, na atafikishwa mahakamani, kuchukuliwa alama za vidole na vile vile  kupigwa picha katika mahakama hiyo kesho Jumanne.

 

 

Mawakili wa Donald Trump tayari wamesema Mteja wao atakanusha mashtaka yote yanayomkabili. Mashtaka haswa yanayomkabili yaliyoorodheswa katika maamuzi ya baraza la juu la mahakama lililoidhinisha kushtakiwa kwake, bado hayajawekwa wazi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!