Home » Harmonize Ataja Siri Ya Uandishi Wa Kazi Zake

Harmonize

Kwa sasa imekuwa ngumu sana kwa msanii na mmiliki wa Kondegang Harmonize kumaliza siku bila ya kuwa katika vichwa vya habari Tanzania. Hii imejiri mara baada ya msanii huyo kutoa siri juu ya mikwaju yake ambayo amekuwa akiiidondosha hivi karibuni.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize kwa mara nyingine tena ameeleza chanzo kikubwa cha uandishi wa nyimbo zake kuwa ni maisha halisi ambayo anayaishi.

 

SOMA PIA:Harmonize Afanya Manunuzi na Mashabiki Zake

 

Katika ngoma ya Single Again, Jeshi amethibitisha ya kuwa mlengwa wa ngoma hiyo ni mpenzi wake ambaye wameachana anayejulikana kwa jina la Kajala Masanja ambaye pia ni mama wa Sosholaiti Paula Kajala.

 

Harmonize aeleza chanzo cha uandishi wake

Siri kubwa katika uandishi wa kazi zake ni pamoja na kuandika vitu vinavyohusu maisha yake ya kila siku yanayomuhusu na kueleza ya kuwa endapo utamtendea wema basi yuko sambamba na wewe na endapo utamtendea ubaya pia lazima utakuta ujumbe wako katika moja ya ngoma zake.

 

Kwa sasa bado mkali huyo kibao cha Single Again anazidi kupeperusha bebdera vyema na ngoma hiyo huku akimtaja Director Kenny kuwa ndiye mtu aliyempendekeza Caren Simba kuwa mlimbwende katika kazi hiyo kutokana na ufanano wake na Kajala.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!