Home » Rayvanny Azidi Kunogewa na Penzi La Fahyma Kwenye Forever

Forever Rayvanny X Fahyma

 

Msanii Rayvanny kutokea Next Level Music amefanikiwa kuachia video yake ya Forever ambayo alitumia muda mrefu kuinadi kwa gharama ambazo aliwekeza katika video hiyo kuwa inafikia kiasi cha milioni 70 za kitanzania.

 

Katika video hiyo iliiyoambatana moja kwa moja pamoja na Audio Vannyboy amemtumia Fahyma ambaye pia ni mama mtoto wake kama mlimbwende katika video hiyo.

 

SOMA PIA:Wizkid Amwonyesha Davido Upendo

 

Ijapokuwa kumekuwa na panda shuka juu kuachana kwa wawili hao lakini bado ujio wa Forever umedhidirisha ya kuwa penzi lao bado linataradadi na uwepo wao utazidi kuendelea.

 

Forever

 

Hii ni kazi ya pili kwa Rayvanny kumtumia Fahyma kama Video Vixen na kazi ya kwanza ikiwa ni Siri ya mwaka 2018 wimbo alioufanya na kumshirikisha Niki wa Pili

 

Katika upande wa Audio ameshiriki Producer Soundboy kutokea Next Level akishirikiana na Mlamon the beats ambaye anafanya kazi chini ya producer S2Kizzy.

 

Moja kwa moja kutoka kwa Director Eris Mzava ndiye muongozaji wa Forever ambaye pia alipitisha mikono yake ya dhahabu katika kazi ya Rayvanny aliyoifanya na Marioo iliyopewa jina la Te Quiero .

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!