Home » Harmonize Afanya Manunuzi na Mashabiki Zake

 

Huwa ni jambo la heri sana pale ambapo wasanii wanapotenga muda wao kwa ajili ya kukutana na mashabiki zao wanaowapa nguvu katika kazi zao za sanaa. Kwa upande wake Jeshi kutokea Kondegang Harmonize yeye siku ya Jumamosi ya Tarehe moja amepata wasaa wa kukutana na mashabiki zake na kufanya manunuzi.

 

SOMA PIA:Harmonize Amsifu Jay Melody

Katika manunuzi hayo yaliyofanyika Vijana Mall jijini Dar es Saalam, Tembo aliambatana na binti ya ZuuKonde huku wakiwa na ulinzi mkali

 

Harmonize

 

Hii ni njia nzuri kwa msanii huyu ambayo hupounguza kiu kwa wapenzi wa muziki wake ambao wamekuwa wakitamani kumuona kutokana na upendo walionao juu yake.

Kwa sasa Harmonize amezidi kutamba na ngoma yake ya Single Again ambayo inazidi kutesa ndani ya Tanzania na hata nje ya mipaka ya Tanzania.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!