Shabiki Ajichora Tatto Ya Uso wa Mungai Eve Kifuani Mwake
Shabiki sugu wa content creator nchini Kenya Mungai Eve amejichora tatoo ya uso wake kwenye kifua chake.
Shabiki huyo alisema mapenzi yake kwa YouTuber yamemfanya achukue hatua ya ujasiri na hatajuta kamwe kuchora uso wake kwenye kifua chake.
Akijibu chapisho hilo kwenye mitandao ya kijamii, Mungai Eve alifurahia mapenzi ambayo shabiki huyo amemwonyesha hata hivyo baadhi ya mashabiki walidai kuwa tattoo hiyo haifanani na Mungai Eve.
“😂😂😂😂huyo ni mimi kweli???I appreciate the love🥹❤️❤️🤗.”
“Kwani kuna Mungai Eve mwingine hatujui?😭😭💀.”
“Hyo ingine utachora karibu na side roho utafute tattoo artist. Hyo tuassume ni rough copy😂.”
“Wah ambia mwenye amekuchora arudishe pesa juu Sasa hiyo ni Nini😂.”
“Nikama alifika halfway akasema hana pesa ya kulipa😂😂.”
“Sasa huyu anaenda hell juu ya bibi ya mtu ….yaani hatukuangi serious Si ungechora yesu atleast utaexplain ukifika paradiso 😂😂😂😂.”
Nchini Kenya, mashabiki wamekuwa wakionyesha mapenzi yao kwa watu mashuhuri wanaowapenda kwa njia sawa.
Mapema mwaka huu, mwanamke aliyetambulika kwa jina la Its Lemarke alijichora tattoo ya jina Azziad mgongoni mwake kama njia ya kuonyesha mapenzi na kumvutia nyota huyo wa Tik Tok.
Shabiki mwingine alinaswa kwenye video akichorwa tattoo ya Uso wa Otile Brown mgongoni mwake. Alikuwa na picha kamili ya msanii ambayo msanii wa tattoo alikuwa akitumia kama mwongozo.
Mwanadada Mkenya ambaye ni shabiki mkubwa wa mwanamuziki Willy Paul pia alifikia kiwango cha juu cha kuchora jina lake kwenye kifua chake. Awali Lizah Njeri alikuwa ameandika bango akikiri mapenzi yake kwa mwanamuziki huyo.
Muda mfupi nyuma, shabiki aliweka Tattoo ya uso wa Diana Marua mgongoni mwake.