Home » Gigy Money Amaliza Tofauti Zake na Moj360

Gigy apatana na Moj360

 

Baada ya tafarani iliyozuka kati ya Gigy Money dhidi ya mzazi mwenzake Mourah, hatimaye tofauti hizo zimefikia mwisho mara baada ya wawili hao kubainisha kupitia Instagram.

 

SOMA PIA:CRDB Wamtangaza Rayvanny Kama Balozi Mpya

 

Jambo hilo litakuwa jema sana kwa wawili haswa kutokana na mtoto ambaye anawaunganisha (Mayra)  ambaye kwa upande wake kuwepo kwa amani baina ya wazazi wake nikitendo bora zaidi ijapokuwa tayari wametengana.

 

Ujumbe wa Gigy kwa Moj360

 

Kupitia ukurasa wa Instagram Gigi Money aliandika kwa urefu juu ya kuwepo kwa uhusiano mzuri baina na wawili hao na kumpa heshima kama baba wa mwanae.

 

Pia kwa upande wa Moj360, yeye alichapisha picha ya Gigy na kuandika ujumbe mfupi uliosema “MalkiaWaNguvu” na kitendo hichi kimeonesha uwepo wa Amani baina yao.

 

Siku chache zilizopita, Gigy pamoja na Moj360 waliingia katika tafrani baina yao ambayo ilizua gumzo katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kufikia hatua ya kupelekana polisi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!