Home » Esma Platnumz, Mwijaku Watia Neno Sakata La Gigy, Moj360

::IIA

 

Tukio la Moj360 kumpelekea polisi Gigy Money nyumbani kwake limezua gumzo hata kwa baadhi ya watu maarufu Tanzania. Mtangazaji wa Clouds Fm Mwijaku pamoja na dada wa msanii Diamond Platnumz, Esma Platnumz wametia neno juu ya jambo hilo.

 

Mwijaku kwa upande wake wakati akiwa anafanyiwa mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari ameeleza kuchukizwa na kitendo hicho cha Moj kumpelekea Gigy Money polisi wakati anafahamu fika ya kuwa kwa sasa Gigy ndiye mtu anayekaa na mtoto wao Mayra na kuhusika katika suala zima la malezi.

 

SOMA PIA:Diamond Platnumz Kuwekeza Katika Sekta Ya Anga Tanzania

 

Mtangazaji huyo pia alichukizwa kwa kutaja ya kuwa hatua aliyoichukua Moj isiwe ni msukumo kutoka kwa mkewe Meena ambaye kwa sasa tayari wameshaanzisha familia na kkumtaja Gigy ya kuw ni wivu ndio unasababisha awe na visa.

 

Kwa upande wake mfanyabiashara Esma Platnumz yeye pia hakufurahiswa na tukio hilo na alijikita zaidi kuongelea kupande wa mahusiano yaliyokwisha kufa na yale mapya ya kuwa si vyema kwa mwanamke kuwa mshawishi kwa mumewe aweze kuleta mitafaruko kwa mtu ambaye alishawahi kuwa na mahusiano naye haswa baada ya kuwa na mtoto anayewaunganisha.

 

Bado hatma na mtafaruko huo hauwawekwa wazi kwa sasa ni wapi umefikia na malezi ya mtoto Mayra ni nani haswa atakuwa na uhalali juu yake kati ya baba yake au mama yake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!