Home » Mo Jay, Gigi Money Wafikishana Polisi

 

Mtangazaji wa kituo cha Radio cha Clouds Fm Moj360 amefikishana pabaya na mzazi mwenzeke Gigy Money mara baada ya mtangazaji huyo kuwasili nyumbani kwa Gigy akifuatana na mkewe Meena pamoja na polisi.

 

SOMA PIA: Video Ya Rara Yamgharimu Zaidi Msanii Phina

 

Chanzo cha sakata hilo ni kitendo cha Gigy kuwa na tabia ya kuingia Instalive na kuanza kumuongelea mzazi mwenzake huyo kwa kutojali malezi ya mtoto wao Mayra ambaye kwa sasa ni Binti mdogo.

 

 

Baada ya hayo pia Gigy alifanikiwa kurekodi kipande kidogo cha timbwili hilo ambalo lilionesha video wakiwa wanatupiana maneno ya ana kwa ana. baada ya muda kupita Gigi alichapisha video katika ukurasa wake wa Instagram ukimuonesha akiwa barabarani akisema kwa muda ule alikuwa akielekea katika kituo cha polisi.

 

Malezi kati ya Moj360 pamoja na Gigy Money yamekuwa moja ya mambo ambayo yamezidi kuzua gumzo katika jamii kutokana na kuwa Mama Mayra mara nyingi hutumia mitandao ya kijamii kuongelea ugumu anaoupata haswa katika suala la malezi baina yake na Baba Mayra.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!