Home » Bondia Karim Mandonga Kutifua Vumbi Na Mganda Jumamosi Jijini Nairobi

Bondia Karim Mandonga Kutifua Vumbi Na Mganda Jumamosi Jijini Nairobi

Mwanamasumbwi tajika wa Tanzania ‘’Karim Mtu Kazi’’ Mandonga  atakuwa akirejea ukumbini wikendi hii jijini Nairobi.

 

 

Mandonga atakabana koo na Mganda Kenneth Lukyamuzi kwa kile Mandonga ametangaza kuwa mechi ya kusisimua na amewaomba wafuasi wake kutokea kwa wingi mno.

 

 

Katika dondi ya raundi hii, Mandonga amesema amekuja na ngumi mpya inyaojulikana kama ‘’Mlunga mbunga’’ kutoka jangwa la sahara kwenye upepo mkali.

 

 

Akicheza na Wanyonyi, Mandonga alimuondoa na ngumi ya Sungunyo.

 

 

Pigano hilo litaandaliwa katika ukumbi wa Kasarani tarehe 25 mach yaani siku ya jumamosi. Mechi hii ya uzani wa kimo utakuwa na raoundi tano.

 

 

Hili litakuwa mara ya pili ya Mandonga kurejea Nairobi baada ya pigano lake na Daniel Wanyonyi ambapo alimlemea kwa ngumi ya TKO

 

 

Mandonga amerejea tena baada ya umma kuitisha pigano hilo. Wana Nairobi walitaka kumuona kwa mchezo tena na tumewaletea mechezo.

 

“Tunatarajia watu kujitokeza kwa wingi kasarani” kasema Seleman Semunyu, mmoja wanaoanda pigano hilo

 

Pigano la Mandonga Mtu kazi na Lukyamuzi ni miongoni mwa pigano kuu Jumamosi. Hata hivyo, pigano kuu litakuwa kati ya mkenya Nick Otieno na Mtanzania Hassan Ndonga. Pigano hilo litakuwa la raundi la nane katika uzani wa super-bantam.

 

Mkenya mwengine Consolata Musanga atakuwa akijaribu kutetea taji lake atakaposhuka dimbani dhidi ya Mtanzania Fatuma Yazidu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!