Home » Joh Makini Afunguka Juu ya Producer Wa Success

 

Mwanamuziki kutokea kundi la Weusi Joh Makini baada ya kuachia EP yake ya Wave yenye ngoma sita, amefunguka juu ya Producer aliyefanya beat ya Success wakati alipofanya mahojiano Fredrick Bundala na katika Simulizi na Sauti.

 

SOMA PIA:Hatimaye Joh Makini Aidondosha Wave

 

Katika mahojiano hayo Joh amemuelezea Jay Raw kama moja kati ya waandaaji wa muziki wenye uwezo mkubwa ambaye alianza kuupenda muziki wa Hip Hop tangu akiwa mdogo na Joh Makini akiwa kati ya watu waliomvutia zaidi kufanya kazi naye.

Katika EP ya mwamba huyu wa Kaskazini yenye jumla ya ngoma sita, Success ni moja ya zile ngoma ambazo zimepata kusifika zaidi  na kupendwa na kundi kubwa la watu ikiongelea maisha pamoja na mafanikio kuwa ni furaha.

 

Mbali na Jay Raw aliyoko katika Extended Playlist ya Wave, kuna wazalishaji wengine wa muziki waliohusika wakiwemo Gachi B, Ammy Waves, Kass pamoja na Nahreel kutokea kundi la Navy Kenzo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!