Home » CCTV Yaonyesha Jinsi Mkenya Irvo Otieno Alivyofariki Marekani

CCTV Yaonyesha Jinsi Mkenya Irvo Otieno Alivyofariki Marekani

Kanda ya CCTV  iliyotolewa na mwendesha mashtaka Jumanne inaonyesha Irvo Otieno akibanwa sakafuni na maafisa wengi wa usalama katika kituo cha afya ya watu waliyo na matatizo ya akili katika jimbo la Virginia katika muda mfupi kabla ya kifo chake mapema mwezi huu.

 

Ofisi ya Mwanasheria wa Jumuiya ya Madola ya Jimbo la Dinwiddie Ann Cabell Baskervill pia ilitoa mawasiliano  kuhusu tukio hilo ambapo mpiga simu aliomba kuletwa kwa ambulensi akisema Otieno hakuwa anapumua.

 

Simu hiyo ya dharura na kanda ya video kwa ujumla yalielezea kwa kina matukio yaliyojiri na kusababisha  kifo cha Otieno mwenye umri wa miaka 28 na mwenye asili ya kiafrika (Kenya). Kwa mujibu wa Baskerville, Otieno alifariki tarehe 6 Machi mwaka huu alipokuwa akihamishwa kutoka jela ya Kaunti ya Henrico hadi Hospitali ya central State

 

 

Kutokana na kisa hicho, maafisa saba wa polisi na wauguzi watatu wa hospitali hiyo wamefunguliwa mashtaka ya mauaji.

Kisa hicho kimewakosesha Familia ya Otieno usingizi na sasa  wanaomba haki kutendeka na wahusika kuadhibiwa vikali kwa mujibu wa sheria.

 

‘’Mwanangu aliachukuliwa kama umbwa, hata vibaya sana kuliko mbaya. Hii niliona ka macho yango mimi mwenyewe’’ alisema mamake otieno

 

 

Otieno alikamatwa na maafisa wa polisi Marekani kutokana na amri ya dharura kwa kuwa ana ugojwa wa akili jambo lililokuwa likimfanya kuwa mwenye fujo wakati mwingine.

 

 

Otieno aliondoka Kenya akiwa na umri wa miaka minne kulekea Marekani ambapo amekuwa akiishi na familia yake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!