Bunge la Uganda Lapitisha Mswada Kali Wa Kuwaadhibu Mashoga
Wabunge nchini Uganda wamepitisha mswada wenye utata dhidi ya LGBTQ+, ambao utafanya vitendo vya ushoga na usagaji kuadhibiwa na adhabu ya kifo au kifungu cha maisha
Hata hivyo mswada huo umeshtumiwa vikali na wanaharakati wa haki.
Kati ya wabunge 389 ni wawili walipinga mswada huo.
Wabunge hao walipiga kura Jumanne jioni ya kupinga LGBTQ ambao unatoa hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa kufanya mapenzi ya jinsia moja na “kuajiri, kukuza na kufadhili’’ shughuli za ushoga na usagaji.
“Mtu anayetenda kosa la ushoga uliokithiri na atawajibika, akipatikana na hatia atauawa,” Kasema Robina Rwakoojo, mwenyekiti wa masuala ya sheria na bunge.
Wabunge wawili tu kutoka chama tawala, Fox Odoi-Oywelowo na Paul Kwizera Bucyana, ndio walipinga sheria hiyo mpya.
“Mswada huo haukutungwa vizuri, una vifungu ambavyo ni kinyume na katiba, unabadilisha mafanikio yaliyopatikana katika vita dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia na kuwafanya watu kuwa wahalifu badala ya tabia ambayo inakiuka kanuni zote za kisheria zinazojulikana,” alisema Odoi-Oywelowo.
“Muswada hauleti nyongeza yoyote ya thamani kwenye kitabu cha sheria na mfumo wa sheria unaopatikana,” alisema.
Mswada huo ni mojawapo ya hatua kali misururu wa vikwazo kwa haki za LGBTQ+barani Afrika, ambapo ushoga ni kinyume cha sheria katika nchi nyingi. Nchini Uganda, nchi yenye Wakristo wa kihafidhina, ngono ya watu wa jinsia moja ilikuwa tayari inaadhibiwa kwa kifungo cha maisha gerezani