Home » Baba Levo Kuachia Extended Playlist

 

Mwanamuziki na mtangazaji kutokea kituo cha redio cha Wasafi Fm Baba Levo ametangaza kuachia EP yake ya kwanza ambayo itakuwa na jumla ya nyimbo saba.

 

SOMA PIA:Meja Kunta Awashirikisha Marioo, Mabantu katika Demu Wangu Remix

 

Mkali huyo wa nyimbo kama Yes No pamoja na High and Low ametoa taarifa hiyo baada ya kuchapisha picha yake katika ukurasa wake wa Instagram kwa kutangaza ya kwamba EP hiyo ataiachia mara baada tu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuisha .

 

 

Ni muda sasa umeshapita tangu msanii huyo aachie kibao baada ya kufanya kazi ya Baikoko kwa takribani miezi mitatu iliyopita na sasa kuachia EP kunaweza kutajwa kama moja ya mafanikio yake ya kimuziki.

 

Mbani na muziki lakini pia Baba Levo tayari alisha wahi kujihusisha na masuala ya kisiasa baada ya kuwa Diwani huko mkoani Kigoma na kwa sasa sanaa na utangazaji ndivyo vitu anavyovifanya katika shughuli za kila siku.

 

 

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!