Home » Tanzania Yatoa Tahadhari Kwa Raia Wake Kufuatia Maandamano Ya Azimio

Tanzania Yatoa Tahadhari Kwa Raia Wake Kufuatia Maandamano Ya Azimio

Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetoa ushauri kwa raia wake nchini Kenya kuwa makini baada ya Azimio kupanga maandamano ya kila siku ya jumatatu na alhamisi.

 

Wizara ya Mambo ya Nje imewataka Watanzania wote wanaoishi nchini Kenya kuchukua tahadhari zote muhimu wanapoendelea na shughuli zao kwa kuzingatia maandamano ya Azimio.

 

 

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje balozi Mindi Kasiga, akizungumza na wanahabari alisema kuwa Watanzania wanaoishi nchini Kenya wanapaswa kuwa na mawasiliano ya karibu na ubalozi wake nchini Kenya, amesema  ubalozi wao utakuwa radhi kutoa  msaada endapo itahitajika.

 

“Ubalozi wetu nchini Kenya chini ya uongozi wa mheshimiwa Simbachawene, anafuatilia hilo swala kwa karibu sana. Kwa kweli Watanzania wachukue tahadhari zote kwa sababu huwezi kujua saa ngapi utakua wapi lakini unavyotoka kwenda kwenye shuguli zako chukua tahadhari za kina kabisa lakini pia uwe na mawasiliano ya karibu na ofisi za ubalozi kwa ajili ya lolote lile,” Alisema

 

Kasinga alikiri kuwa Kenya ni mwenyeji wa jumuiya kubwa ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi ambao wanajihusisha zaidi na biashara, na kuwataka kutumia simu iliyotolewa na Ubalozi wa nchi hiyo iwapo watahitaji msaada wowote.

 

“Tuna diaspora kubwa sana ya Watanzania nchini Kenya na wako katika maeneo tofauti lakini wengi wao ni wafanya biashara ambao wanaendesha shughuli za biashara kule. Kwa hivyo tunachowaomba na kuwashihi ni kuwa makini kuchukua tahadhari zinazotolewa na pia kuweka mahusiano ya karibu. ya hotline pale ubalozini wawe karibu, wakipata matatizo yoyote, saa yoyote wawepo na namba hiyo karibu ili waweze kupewa msaada,” alisema.

 

Mkurugenzi wa mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya nje alisema hatarajii vurugu zozote kuzuka Mombasa, na kuongeza kuwa iwapo machafuko yatatokea, Watanzania wanaweza kutafuta usaidizi kutoka kwa ubalozi mdogo wa nchi hiyo katika jiji la pwani.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!