Home » Maafisa 24 Walijeruhiwa Wakati Wa Maandamano

Maafisa 24 Walijeruhiwa Wakati Wa Maandamano

Inspekta Generali wa polisi Japhet koome amesema watu 213 wamekamatwa katika jiji la Nairobi  na kisumu na maafisa polisi 24 kujeruhiwa. Maandamano hayo yaliofanyika kupinga ongezeko la gharama za maisha nchini yalisababisha maafisa 31 wa polisi kujeruhiwa.

 

katika maandamano ya jumatatu, Polisi walitumia mabomu ya kutowa machozi na mabomba ya maji dhidi ya waandamanaji ambao baadhi walikuwa wakirusha mawe na kuchoma moto matairi. Polisi pia walifyetua mabomu ya kutowa machozi dhidi ya msafara wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliyeitisha maandamano hayo nchi nzima.

 

Machafuko yaliyoshuhudiwa jana nchini Kenya yalikuwa mabaya zaidi kuwahi kuonekana tangu alipoingia madarakani William Ruto miezi sita iliyopita baada ya kumshinda kwenye uchaguzi Raila Odinga.

 

 

Koome ameongeza kusema uchunguzi bado unaendelea ya kuwasaka wale wote waliyohisika na fujo, uharibifu wa mali, wizi na vurugu ya aina yeyote. amesema watahakikisha wamechukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!