Home » Maandamano Ya Kitaifa Yazidi Kuchacha Afrika Kusini

Maandamano Ya Kitaifa Yazidi Kuchacha Afrika Kusini

Maandamano yakiendelea kupamba moto nchini Kenya, Afrika Kusini mambo ni kama hayo baada ya waandamanaji kujitokeza katika miji kadhaa katika taifa hilo kufanya maamdamano ya amani.

 

Kulingana na polisi, watu zaidi ya  87 wamekamatwa kote nchini kufuatia  maandamano ya upinzani ambayo awali ilitajwa haramu.

 

 

Maandamano hayo yalikuwa yameitishwa na Kiongozi wa Upinzani, Julius Malema. Mkuu wa polisi Bheki Cele amesema waliokamatwa wengi wao ni kutoka katika mji wa Gauteng.

 

Cele amedai zaidi ya magurudumu 25,000 yalizuiliwa na polisi katika miji kadhaa Afrika kusini.

 

Ameongeza kusema  polisi wanashirikiana na wanajeshi kuimarisha usalama na kurejesha utulivu.

 

Economic Freedom Fighters (EFF) kinasema kinaongoza kile kinachoitwa ‘kufungwa kwa shughuli za kitaifa’.

 

Maandamano  ilianza Jumapili saa sita usiku na kitamalizika jumatatu usiku wa manane.

 

EFF kinatoa wito wa kujiuzulu kwa Rais Cyril Ramaphosa na kumalizika kwa mzozo wa nishati nchini humo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!