Home » Watu 2 Wauwawa West Pokot Na Mifugo 150 Kuibwa Samburu

Watu 2 Wauwawa West Pokot Na Mifugo 150 Kuibwa Samburu

Watu wawili wameuwawa chini ya siku mbili West Pokot huku mmoja akiuguza majeraha ya risasi baada ya kuvamiwa katika kijiji cha Lower Mara eneo la Longewan Samburu magharibi. Kwenye uvamizi huo uliofanyika saa kumi alfajiri, mifugo 150 waliibwa.

 

Hali ya usalama inaendelea kudorora katika kaunti ya Samburu, hii ni baada ya jamaa moja kumiminiwa risasi na wavamizi alipojaribu kuwazuia kuiba mifugo yake.  Jamaa huyo kwa sasa anauguza majeraha katika kaunti ya Samburu. Katika uvamizi huo, mifugo wake zaidi ya 150 waliibwa.

 

Wanakijiji waliovamiawa ni baadhi ya watu walioamrishwa kuhamia maeneo salama na waziri wa usalama Prof. Kithure Kindiki.

 

 

Uvamizi huu unawadia tu siku chache baada ya serikali ya Kenya kuanzisha oparesheni kali ya kuwafukuza wavamizi na wezi wa mifugo maeneo ya kaskanini mwa bonde la ufa.

 

 

Baadhi za maeneo zilizoathirika ni kaunti za Samburu, Turkana, West Pokot, Baringo na Laikipia.

 

 

Wavamizi hao wamekuwa wakiwahangaisha wananchi maeneo hayo kwa muda sasa na kukwamisha shughuli nyingi kama vile masomo, ustawi wa maeneo hayo na kuchangia kudorora kwa usalama.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!