Home » Anerlisa Muigai: Wacheni Kuniomba Namba

Mrembo Mrithi wa kampuni ya vileo ya Keroche Anerlisa Muigai amewaeleza mashabiki wake jinsi ya kuzungumza na kuelewana naye iwapo watakutana hadharani.

 

Kupitia insta stories, Anerlisa ameleezea masikitiko yake kutokana na majibizano ya hapo awali na mashabiki akisema alihitaji kuyasema kwani mengi ya maelezo yake yanafuatiliwa na watu mashuhuri.

 

“Nilidhani ni lazima niweke wazi kwa sababu najua watu wengi wa umma wangekubaliana nami,” alisema.

 

Anerlisa alisema ukikutana naye, itakuwa busara kumpatia kadi yako ya biashara pekee.

 

“Ni uungwana kuacha kuomba namba binafsi kwa sababu tu tumekutana hadharani, juzi nilitoa namba yangu kwa dem fulani ambaye aling’ang’ania sana ya kibinafsi na kuikataa ya ofisi, sasa WhatsApp yangu imejaa CV.

 

“Njia nzuri ya kufanya hivyo ni kumpa mtu kadi yako na akikupigia basi ujue alikuwa na nia ya kujua nia yako, kama huna kadi tafadhali usitake namba za simu.,” alisema.

 

Zaidi ya hayo, amewaonya wamiliki wa biashara kutumia picha zake kutangaza biashara zao. Hii, alibainisha ni kwa misingi kwamba wanaruhusiwa kutumia iwapo kuna makubaliano.

 

Alisema kuwa ukurasa wake una wafuasi zaidi ya milioni moja na unatosha kwa biashara iwapo mtu anataka kutangaza.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!