Gianni Infatino Ateuliwa Tena Kuwa Rias Wa FIFA
Gianni Infantino ameteuliwa bila kupingwa kama rais wa shirikisho la soka duniani FIFA
Infatino atahudumu tena kama rais wa FIFA muhula wa miaka minne hadi mwaka 2027.
Raia huyo wa uswizi mwenye umri wa miaka 52, alithibitishwa kuendelea na wadhifa wake huo kwa shangwe katika kongamano la FIFA linalofanyika mjini Kigali, Rwanda.
Punde tu baada ya kuteuliwa tena, amesema ni heshima na fursa kubwa, lakini pia ni wajibu mkubwa na kwamba watu waendelee kuamini ahadi yake.
Infantino alithibitisha kiwango cha rekodi ya mapato ya fifa katika mzunguko uliopita kutoka 2019-22, lakini ameahidi kuongeza hii tena kwa msingi wa mashindano yaliyopanuliwa ya kombe la dunia la wanaume na wanawake na kuanzishwa.
Awali, alizindua uwanja wa pele, kwa heshima ya sogora wa soka wa brazil aliyefariki desemba mwaka jana.
Uwanja ulijulikana kama uwanja wa mkoa wa Kigali yenye idadi ya mashabiki 22,000.
Uzinduzi huo uliongozwa na rais Wa Rwanda Paul Kagame.
Rais Kagame alimshukuru Bw. Infantino kwa kuipa nchi fursa ya kumheshimu Bw. pele kwa kuutaja uwanja huo kwa jina lake.