Home » Huddah Monroe: Wanaume Wakenya Ni Stingy

Sosholaiti Huddah Monroe amewakashifu wanaume Wakenya wanaomtaka lakini ni ‘stingy “ na wabahili.

 

Katika video ya hivi majuzi kwenye mtandao wake wa Instagram, Huddah alisema hajawahi kuelewa ikiwa wanaume wa Kenya ni stingy ama hawapendi kutoa hela zao.

 

Kulingana na Huddah, wanaume wanaotaka kuwa naye, wanapaswa angalau kutuma pesa za mafuta ya gari lake au hata kum-spoil na pesa.

 

“Unataka kukaa nami, kunywa kinywaji na mimi au kunifahamu na Huwezi kunitumia pesa za mafuta ya gari langu au hata kununua lipstick wewe ni wa nini sasa ,” alisema.

 

Huddah aliongeza kuwa hata mpenzi wake wa zamani alikuwa akimnunulia vitu kwa kidogo alichokuwa nacho.

 

Huddah alidai kuwa baadhi ya wanaume ni mabilionea lakini hawawezi kutumia pesa hizo kwa watu lakini walizipata kinyume cha sheria.

 

“Unaibia serikali bado hutaki kutoa hizo pesa. Utakufa na kuacha hizo pesa sikia. Unaenda likizo Dubai mara moja kwa mwaka na bado una pesa heehe wakenya.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!