Home » Abigail Chams Kuachia Video Ya Nani

 

Kibonde wa kibao cha Nani Abigail Chamz ametangaza kudondosha  video ya ngoma hiyo siku ya Jumatano ambayo amemshirikisha Marioo ambaye kwa sasa bado anatamba na albumu yake ya The Kid You Know.

 

SOMA PIA: Navy Kenzo Waachilia Albamu Mpya

 

Kwa ushirikiano na Applemusic Abby ametambulishaa uzinduzi huo alioupa jina la THE DOTTY SHOW na kwa sasa mwanadada huyo amekuwa akiendeleza harakati zake za kujitambulisha kimuziki katika upana wa kimataifa zaidi.

 

Mbali na uzinduzi wa Video hiyo ya Nani, wawili hao pia waliokutana katika ngoma hiyo wanasemekana kuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa sasa na hicho kikiwa ndiyo chanzo cha ukaribu wao.

 

Abby tayari ameshafanya ngoma mbalimbali na wasanii wakubwa wa bongo akiwemo Konde boy katika wimbo wa Leave Me Alone ambao umefanya vizuri katika majukwaa makubwa ya muziki.

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!