Home » Ali Kiba Alamba Shavu Albumu Ya Davido

Ali Kiba Miongoni mwa wasanii kwenye Album ya Davido

 

Mkali wa kibao cha Mahaba King Ali Kiba alamba shavu katika albumu ya Davido albumu iliyopewa jina la Imagination Wan Kill Me msanii kutokea Nigeria mara  baada ya orodha ya albumu hiyo kusambaa ikiwa na jumla ya ngoma 17 na katika nyimbo hizo King Kiba ni moja ya wasanii walioorodheshwa.

 

SOMA PIA: Harmonize Aanzisha Podcast

Katika albumu hiyo wasanii mbalimbali wakubwa duniani na Afrika wameorodheshwa na wasanii hao ni pamoja na Black Sherif, Seyi Vibes, Pheels, Dremo,  Wizkid, SZA, Travis Scott, Ali Kiba pamoja na wasanii wengine.

 

Ujio wa albumu hiyo ulihairishwa baada ya kifo cha mtoto wa Davido kilichomfanya akae kimya na kupeleka mbele ujio wa albumu  yake hiyo.

 

Mbali na hilo, Davido pia katika akaunti yake ya Instagram ameondoa picha zilizokuwa katika ukurasa wake huo na kuacha picha tatu pekee na huendi huu ndio ujio wa mwamba huyo kutokea Nigeria.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!