Home » Ruby Apata Mtoto Wa Pili

 

Staa wa muziki kutokea Tanzania Hellen Majeshi (Ruby) amefanikiwa kupata mtoto wa pili hivi karibuni. Ujio huo wa kichangaa hicho umethibitishwa na picha ambayo mwanamuziki huyo ameichapisha kupitia ukirasa wake wa Instagram ikionesha miguu ya mtoto ikiambatana na ujumbe uliosema

 

 

“Little feet that kicked my bell so much…. my G is here…”

 

Mwanamuziki huyo amefanikiwa kupata mtoto huyo na Ebenhard Nation ambaye pia anajulikana kwa jina la Ebenation ambaye pia ni mbobezi wa masuala ya muziki biashara.

 

SOMA PIA: Navy Kenzo Waachilia Albamu Mpya

 

Ruby aliutambulisha umma juu ya ujauzito wake mwezi Januari baada ya kuchapisha picha mbalimbali zilizomuonesha akiwa na ujauzito katika akaunti zake za mitandao ya kijamii.

 

Huyu ni  mtoto wa pili kwa Ruby mara baada ya kufanikiwa kupata mtoto wa kwanza na mzazi mwenza wake Kusah ambaye pia ni mwanamuziki wa BongoFleva.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!