Home » Mke wa Msanii Guardian Angel, Esther Musila Adai Kutongozwa Sana

Esther Musila, mke wa msanii wa injili Guardian Angel ameelezea jinsi watu wanavyoshindwa kuheshimu taasisi ya ndoa.
Esther Musila amesema DM yake imejaa wanaume wanaomtaka kimapenzi licha ya kufahamu kuwa ameolewa na Guardian Angel.

 

Kulingana na Musila hana nafasi ya mtu mwingine na wakati mwingine yeye hupuuza au kufuta jumbe hizo.
” The ones that are are extreme, I delete and block.”
Guardian Angel alisema pia anashinikizwa kuoa mke wa pili kitu ambacho hataki kujihusisha nacho.
” I have a wife and I have seen how it is for people who decided to be polygamous. I believe that is something I wouldn’t tolerate. One wife is enough and I am able to concentrate better with one.”

 

Musila na Guardian Angel waligonga vichwa vya habari kutokana na tofauti yao ya umri jambo ambalo lilizua mjadala mkali miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

 

Mapenzi yao yanaendelea kuenda viwango tofauti kila mwaka zaidi na wawili hao sasa wamekuwa miongoni mwa wanandoa wanaosherehekewa zaidi mjini.

 

Mnamo Januari, wanandoa hao kwenye mitandao ya kijamii walisherehekea umbali ambao wametoka kwani Guardiana Angel pia aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya miaka 35.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!