Diamond Platnumz Ashangazwa Na Mabadiliko Ya Uzani

Uzani wa Mwanamziki nyota wa bong Diamond unaendelea kuzua mjadala miogoni mwa mashabiki zake.
Haya yanajiri wakati ambapo kumekuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu mwili wa staa huyo wa Bongo.
Siku za hivi karibuni baadhi ya mashabiki wamekuwa wakihoji afya ya mwimbaji huyo huku wakidai kuwa anaonekana mwembamba kupita kawaida.
“Ipo siku tutakutana kujadili afya ya huyu mtu, nipo hapa,” aliandika mtumiaji mmoja wa Instagram chini ya chapisho la hivi karibuni la Diamond kwenye mtandao huo.
Maoni mengine mengi yanayofanana na hayo yameonekana katika chapisho mengine kwenye kurasa zake mbalimbali za mitandao ya kijamii.
Hivi karibuni bosi huyo wa WCB alidokeza kuwa ugomvi wake wa muda mrefu na mwimbaji mwenzake Alikiba umefikia mwisho.
Staa huyo alidokeza kuwa kwa sasa hali ni shwari kabisa kati yake na Alikiba huku akionyesha mapenzi makubwa kwenye mtandao wa Instagram.
Siku ya Jumapili, Diamond alikiri kuupenda sana wimbo wa ‘Asali’ alioutoa Septemba mwaka jana.
Aliweka wazi kuwa ni kibao alichopenda Alikiba. “Favourite 🏆” Diamond aliandika chini ya picha ya bango la wimbo wa Alikiba.
Wengi wamechukua hatua hiyo ikiwa ni ishara kuwa Diamond hana kinyongo na mwimbaji mwenzake.
Wasanii hao wawili wakongwe wa muziki Bongo, wamedaiwa kuwa na ishu kwa muda mrefu na mara kadhaa wamekuwa wakionyesha wazi chuki zao, hata hivyo ni mara chache sana wamekuwa wakizungumzia tofauti zao.
Katika wimbo wa ‘Nawaza’ aliyoutoa mapema mwaka jana, Diamond alikiri kuwa baada ya kutafakari kwa kina aligundua kuwa yeye na Alikiba wanatofautiana katika mambo madogo madogo kama mashabiki na umaarufu.
Bosi huyo wa WCB alizidi kubainisha kuwa amekulia kwenye tasnia ya muziki na hajishughulishi tena na masuala hayo.
I have not checked in here for a while as I thought it was getting boring, but the last several posts are great quality so I guess I’ll add you back to my everyday bloglist. You deserve it my friend 🙂