Home » Gidi Afichua Kilichomfanya Apoteze Uzani

Mtangazaji maarufu wa kipindi maarufu cha Redio cha Gidi na Ghost asubuhi kinachopeperushwa na Radio moja humu nchini, Joseph Ogidi almaarufu Gidi Gidi amekiri kuwa amepungua uzito wa mwili siku za hivi karibuni.

 

Katika maelezo yake siku ya Jumanne, Gidi amefichua kuwa alikuwa mgonjwa kwa muda katika siku chache zilizopita.

 

Mtangazaji huyo mahiri hata hivyo aliweka wazi kuwa cha kushukuru, sasa amepona kabisa.

 

“Habari za asubuhi, ndiyo nimepungua kilo kadhaa, nilikuwa mgonjwa lakini sasa nimepata nafuu,” alisema kupitia Instagram.

 

Kufuatia hayo, Gidi alitoa shukrani zake za dhati kwa Mungu kwa kumwezesha kupata afya njema baada ya kuugua.

 

Alidokeza kuwa aliugua baada ya kula chakula kibovu na hivyo kuwaonya watu kuwa makini na wanachokula. “Kuwa mwangalifu na uangalie kile unachokula, sumu ya chakula ni kweli,” alisema.

 

Takriban wiki tatu zilizopita, Gidi alifichua kwamba alikuwa amelazwa hospitalini baada ya kuugua.

 

Katika ukurasa wake wa Instagram, mtangazaji huyo alichapisha picha yake akiwa katika chumba cha hospitali akiwa na sindano kwenye mkono wake wa kushoto na kubainisha kuwa alikuwa akipata nafuu.

 

 

“Siku ya tatu ya sindano ya 5, ninahisi vizuri,” alisema kwenye ukurasa wake wa Instagram. Kwa siku mbili, mashabiki wa kipindi maarufu cha Gidi na Ghost walikosa sauti yake huku mtangazaji mwenzake Ghost Mulee akiendesha kipindi peke yake.

 

Wakati huo, Ghost alifichua kuwa mwenzake alikuwa amepumzika kidogo na kudokeza kwamba angerejea baada ya siku chache.

 

 

“Leo hatuko na bosi wangu. Kesho (Ijumaa) hatutakuwa naye pia. Bosi wangu amepumzika kidogo. Natumai tutakuwa naye Jumatatu,” Ghost alisema wakati wa kikao cha asubuhi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!