Xtian Dela Atoa Sababu Ya Kutorudi Nyumbani Kwa Miaka 4
Mwanablogu Xtian Dela bado anajadiliwa tena baada ya mama yake kujitokeza kumsihi arudi kwa familia yake.
Kulingana na mamake, Xtian aliondoka na kukata mawasiliano nao miaka minne iliyopita na tangu wakati huo wamekuwa wakijaribu kumtafuta.
Mchungaji Naomi Nyongesa aliongeza kuwa hata ndugu wa Xtian wamejaribu kumfikia lakini jitihada zao zote zimeambulia patupu.
Alichobaki nacho sasa ni kumbukumbu nzuri za jinsi alivyomwona mwanawe akijenga tasmia yake katika burudani na kujitengenezea nafasi.
Anasema matatizo yalianza pale alipoanza kukosoa maisha yake ya starehe na kujichora tattoo mwilini mwake. Hata hivyo, anasema alikuwa akijaribu tu kumwangalia mwanawe na hakuwa na nia mbaya.
Dela amejibu madai hayo kwa kuchapisha makala ambayo yanayozungumzia wazazi wenye hulka ya kuangazia wanao na sifa zao ambazo ni pamoja na, kubadilisha tabia, na ukosefu wa mipaka miongoni mwa mengine.
Wakenya kwenye Twitter hawakukosa maoni kamwe kuhusu suala hilo. Wengine wakimuunga mkono Xtian, wengine wameegemea upande wa mamake.
Miezi kadhaa iliyopita Dela alijitokeza kupitia mitandao yake ya kijamii akidai kuwa alikuwa amekata tamaa na anahitaji msaada. Xtian amekuwa na msongo wa mawazo kufuatia kufutwa kwa akaunti yake ya Instagram iliyokuwa na wafuasi zaidi ya milioni moja.
Sababu ya kughairiwa kwake, alisema ilikuwa nje ya miongozo ya kijamii ya mtandao huo.
Dela alikuwa akiendesha kitengo Fulani kiitwachwo Toboa ambapo angechapisha maswala yaliyotumwa kwake na watu kuhusu matukio yao ya ngono.
Akaunti hiyo ilikuwa muhimu kwake kwa sababu haikuwa akaunti tu bali jukwaa ambalo lilikuwa likimuingizia kipato kupitia matangazo.
Mwanabloga huyo amekuwa msisimko kwenye mitandao ya kijamii kwa miaka mingi. Mwanzoni mwa covid, Dela alikuja na kipindi cha mtandaoni kilichopewa jina la klabu covid ambacho alijikuta akizozana na sheria kutokana na maudhui ya wazi yaliyokuwa yakipeperushwa.
Mwanamuziki huyo hata hivyo alidai kuwa onyesho hilo lilimletea zaidi ya shilingi milioni sita za Kenya.