Home » Wakenya Waonyesha Wanaovyomwenzi Ayra Starr Kutoka Nigeria

Wakenya Waonyesha Wanaovyomwenzi Ayra Starr Kutoka Nigeria

Mwimbaji wa nyimbo za kisasa kutoka Nigeria Oyinkansola Sarah Aderibigbe, maarufu kama Arya Starr aliongoza tamasha la Shoke Shoke lililosisimua umati wa vijana katika KICC Nairobi Wikendi hii.

 

Maelfu ya mashabiki walipamba hafla hiyo katikati mwa jiji kuu la Kenya huku kila mmoja akiburudika hadi saa kumi na moja za asubuhi siku iliyofuata.

 

Wanamuziki wa humu nchini Khaligraph Jones, Mejja, na Rosa walikuwa miongoni mwa wale ambao pia waliwatumbuiza umati huo.
Waliohudhuria ni akiwemo gavana Johnson Sakaja, mbunge wa Lang’ata Felix Odiwuor ‘Jalang’o na mwanahabari Shaffie Weru.

 

“Nimefurahi kuwa hapa pamoja nanyi usiku wa leo na ninaweza kuthibitisha kwamba sote tumefurahia. Nairobi ni jiji la vijana na ubunifu. Hivi majuzi niliwaomba content creators wote wajisikie huru na (CBD) wanapokuwa katika majukumu yao. Hakuna mtu atakayekusumbua. Tunatafuta njia zaidi za kukuunga mkono,” alisema Sakaja.

 

 

Hafla hiyo pia ilitumika kuhamasisha umma juu ya hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa huku waandaaji wakipanda miti 1000..

 

Milango ilifunguliwa saa 4:00 jioni huku burudani ikianza saa mbili baadaye kutoka kwa ma-DJ kadhaa kabla ya Ma –MC’s maarufu kama washereheshaji wa usiku huo kupanda jukwaani.

 

Msanii huyo wa kibao cha ‘Rush’ alipanda jukwaani huku mashabiki waliokuwa wakimshangilia kwa kipindi kizima cha onyesho lake lililodumu kidogo kwa saa moja.

 

Alishiriki jukwaa na msanii mwenza Bayanni mtunzi wa wimbo wa ‘Ta Ta Ta’.

 

Kisha alithamini upendo kutoka kwa mashabiki wake na akaeleza jinsi alivyohisi hisia nchini Kenya.

 

“Nairobi ni jiji zuri na kuwa hapa kunanifurahisha sana. Asanteni Kenya na ninawaahidi kila mmoja wenu kuwa mtaniona zaidi katika miezi ijayo,” Ayra Star.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!