Home » Zuchu Adai Aliwahi Kudhulumiwa Mwanzoni Mwa Safari Yake Ya Muziki

Msanii chipukizi kutoka Bongo Fleva Zuchu ameachia single yake mpya inaitwa “Napambana”. Huu ni wimbo ambao unaongelea mapambano kwenye maisha ya kila siku.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ametupa hadithi fupi kuhusiana na wimbo huo na kusema kuwa aliandika wimbo huo kipindi ambacho alikuwa akipitia kipindi kigumu cha kifedha.

 

Mrembo huyo kutoka WCB amesema kuwa alinyimwa haki yake na mtu wakati alikuwa amefanya kazi.

 

“Niliandika huu wimbo takribani mwaka na miezi kadhaa umepita. Wimbo niliandika kwa sababu nilikua napitia Matatizo ya kifedha kidogo nikanyimwa haki yangu na mtu ilhali kazi nilifanya” Aliandika.

 

Utakumbukwa napambana ni wimbo wa pili kutoka kwa Zuchu mwaka 2023 baada ya Utaniua.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!