Home » Nyufa Zaibuka Kenya Kwanza

Mkakati wa Rais William Ruto wa kuunganisha vyama tanzu vya Kenya Kwanza na chama cha (UDA) kwa mara ya kwanza umekabiliwa na upinzani huku baadhi ya washirika wakipinga hatua hiyo.

 

Akizungumza na wanahabari leo hii jumamosi, katibu mkuu wa Chama cha Democratic, Jacob Haji, ameshikilia kuwa hawatakubali shinikizo la kujiunga na UDA.

 

Afisa huyo ambaye ni mwandani wa kiongozi wa chama hicho ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu, Justin Muturi, ameeleza kuwa chama tawala kinahitaji kuafiki pande zote na kukuza demokrasia ya vyama vingi.

 

Kauli ya Haji inajiri baada ya Katibu Mkuu wa UDA, Cleophas Malala kufichua mipango ya kushirikiana na vyama mballimbali ndani ya muungano huo kujiunga na UDA.

 

Malala alieleza kuwa hatua hiyo itaimarisha timu ya Kenya Kwanza, na kuifanya iwe hai zaidi.

 

Kwa upande mwingine, alipokuwa akizungumza mjini Eldoret jana , Naibu Rais Rigathi Gachagua alieleza kuwa Malala aliteuliwa kuleta msisimko kwa chama tawala huku wakipanga mikakati ya uchaguzi ujao.

Aidha mpango mpya wa UDA ulitumiwa mwaka wa 2017 na aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta ambaye alipanga vyama tanzu kuwa chama kimoja cha Jubilee.

 

Wakati huo huo, UDA imetangaza kuandikisha kwa wingi wanachama wake wapya kabla ya uchaguzi wa kitaifa wa viongozi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!