Mahojiano Ya Makatibu Wakuu Tawala Yaanza
Mahojiano ya wagombeaji walioteuliwa kwa nyadhifa za Katibu Mkuu wa Tawala (CAS) yameanza leo Jumatano.
Wagombea 240 walioteuliwa watahojiwa na Tume ya Utumishi wa Umma uhakiki uliaonza leo Machi 1 hadi Machi 7.
Wagombea waliopangwa kufika ni pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu Fred Segor, aliyekuwa kamishna wa IEBC Thomas Lentangule, Isaac Mwaura, Denis Itumbi, Simon Mbugua, Jeremiah Ruto na Wilson Sossion.
Msimamo wa serikali kuhusiana na wadhifa huo ulianzishwa mwaka wa 2018 kama sehemu ya juhudi za serikali za kurahisisha usimamizi wa masuala ya umma.
Majukumu mahususi ya katibu mkuu tawala yanaweza kutofautiana kutegemea na wadhifa waliopewa, lakini kwa ujumla, wanatarajiwa kumsaidia waiziri katika kuunda na kutekeleza sera katika wizara zao, kumwakilisha waziri huyo katika shughuli na mikutano rasmi kama ilivyopangwa..
Pia wanashughulikia miradi maalum kama itakavyoagizwa na waziri, kutoa mwelekeo katika usimamizi wa shughuli za wizara na kuwasiliana na wadau, ikiwa ni pamoja na mashirika mengine ya serikali, sekta binafsi, na mashirika ya kiraia, kwa niaba ya waziri.
Jukumu hili linatoa daraja kati ya waziri na wafanyikazi wengine wa wizara, kuhakikisha kuwa maamuzi ya sera yanawasilishwa na kutekelezwa ipasavyo.
Wagombea wanatakiwa kuja na vyeti halisi, pamoja na vyeti vya idhini kutoka kwa idara mbalimbali kama vile ile ya ushuru KRA, HELB, Ofisi ya Marejeleo ya Mikopo iliyosajiliwa, cheti cha kibali cha polisi, fomu iliyotiwa saini na EACC wakati wa mahojiano.
Wakenya pia wamealikwa kuwasilisha taarifa zozote za kuaminika kuhusu wagombea walioteuliwa Mara baada ya usaili kukamilika, wagombeaji waliofaulu watakabidhiwa kwa rais ili kuteuliwa.
Serikali iliyopita chini ya Rais Uhuru Kenyatta ilikuwa na makatibu wakuu wa utawala 17.