Home » Baraza La Mawaziri Lawazuia Wafanyakazi Wote Wa Serikali Kuendesha Biashara Za Kibinafsi

Baraza La Mawaziri Lawazuia Wafanyakazi Wote Wa Serikali Kuendesha Biashara Za Kibinafsi

Kupitia mkutano uliongoozwa na rais Wiliaim Ruto wa Baraza la Mawaziri, umeidhinisha mswada unaotaka kupunguza ushiriki wa wafanyikazi wa umma katika biashara za kibinafsi.

 

Uamuzi huo ulitolewa wakati wa kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Mkuu wa Nchi kilichofanyika Ikulu ya Nairobi.

 

Kulingana na mkutano huo, mswada uliopendekezwa utasaidia kuzuia mvutano na mgongano unaoweza kujitokeza kati ya masilahi ya kibinafsi na kutekeleza majukumu yao rasmi.

 

Rais Ruto na baraza lake la mawaziri wamethibitisha kuwa mswada huo ni sehemu ya ahadi yao ya kukuza utawala bora na maadili ya kitaifa.
Mswada huo, ukishapitishwa na kuwa sheria, utatoa mfumo wa usimamizi wa kimaslahi inayoweza kuwazuia maafisa wa serikali kuzingatia kikamilifu majukumu yao ambayo kulingana nao yamesababisha visa vingi ambavyo haviendani na azma ya serikali.

 

Aidha, Baraza la Mawaziri lilipitia uamuzi wa awali wa Baraza la Mawaziri wa 1971 wa kupitisha Ripoti ya “Tume ya Ndegwa”  ambayo iliruhusu watumishi wa umma kuwa na uwezo wa kujihusisha na maslahi binafsi na masuala ya kibiashara.

 

Aidha, baada ya kujadiliwa hapo jana. Mswada huo utapelekwa bungeni ili kuangaziwa kwa kuzingatia mchakato uliowekwa kwenye katiba.

 

Wasiwasi kuhusu maafisa wa umma wanaojihusisha na biashara za kibinafsi kwa gharama ya utoaji wa huduma umeibuliwa hapo awali.

 

Kesi za maafisa wa serikali kufuatilia na kushawishi utoaji wa zabuni kwa kutumia uwezo wao pia zimekuwa zikiangaziwa hapo awali katika kile kilichoonekana kuwa njia kuu ya ufisadi.

 

Mnamo 2019, baraza la mawaziri wa aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta lilipendekeza mswada ambao ungewaruhusu wafanyikazi wa umma kutangaza utajiri wao, ikiwa ni pamoja na mapato ya kukodisha, mapato ya biashara, mapato ya kilimo na uwekezaji.

 

Mswada huo ulibuniwa kama sehemu ya juhudi za serikali za kupunguza visa vya ufisadi na ubadhirifu hasa kupitia maslahi yanayokinzana.

 

Makatibu wote wa baraza la mawaziri na maafisa wa umma, kulingana na pendekezo hilo, watawasilisha hoja kwa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kwa madhumuni ya marejeleo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!