Home » Hazina Ya Kitaifa Inatatiza Ukuaji Katika Kaunti, Wasema Magavana

Hazina Ya Kitaifa Inatatiza Ukuaji Katika Kaunti, Wasema Magavana

Magavana wamelaumu kutokuwa na uwezo wao wa kuwekeza katika miradi ya maendeleo katika kaunti zao kutokana na utoaji wa fedha usiofuata utaratibu na Hazina ya Kitaifa.

 

Magavana amesema kushindwa kwa Hazina kufuata ratiba ya utoaji pesa kumeathiri utekelezwaji wa programu za kaunti kwa wakati.
Aidha wakuu hao wa kaunti mbalimbali wamekuwa wanajibu madai ya Mdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakang’o akiwashutumu kwa kukiuka sheria inayotaka angalau asilimia 30 ya bajeti ya serikali ya kaunti itengewe matumizi ya maendeleo.

 

Ripoti hiyo inasema kwamba, ingawa hakuna kaunti iliyoafiki kizingiti cha kisheria cha kukabidhi angalau asilimia 30 ya rasilimali kwenye bajeti ya maendeleo, karibu nusu ilikiuka mahitaji ya viwango vya karibu asilimia 4.

 

Akizungumza baada ya mkutano wa Baraza la Magavana katika hoteli ya Pride Inn Flamingo mjini Mombasa, Gavana wa Nandi Stephen Sang amesema kaunti zimeangazia zaidi kulipa mishahara.

 

Kaunti 10 bora, kulingana na ripoti ya mdibiti wa bajeti Nyakang’o zilitumia kati ya Sh12 na Sh20 kwa matumizi ya kawaida kwa kila shilingi iliyowekwa katika maendeleo, zaidi ya kiwango cha kisheria cha Sh2.33.

 

Kaunti hizo ni pamoja na Kiambu ambapo gavana wake ni Kimani Wamatangi (Sh19.9), Kitui ambaye gavana wake ni Julius Malombe (Sh19), Bungoma ambaye gavana wake ni Ken Lusaka na Kaunti ya Makueni ya Mutula Kilonzo Jr (Sh17).

 

Gavana Kilonzo Jr kwa upande wake amesema kaunti zinakabiliwa na matatizo ya pesa ambayo yamelemaza huduma na miradi iliyokwama.
Kilonzo Jr amelazimika kufanya mazungumzo na Mamlaka ya Usambazaji wa Dawa na vifa KEMSA ili kusambaza dawa katika kaunti yake licha ya kushindwa kulipa shirika hilo kwa bidhaa zilizotolewa Juni mwaka jana.

 

Amelitaka Bunge lishurutishe Waziri wa Hazina Njuguna Ndung’u kufuata ratiba ya utozaji iliyowekwa na Seneti.

 

Spika wa Seneti Amason Kingi amelalamikia kucheleweshwa kwa kutoa pesa kwa kaunti akisema, kunaathiri vitengo vilivyogatuliwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!