Baraza La Mawaziri Ladhinisha Uzinduzi Wa Vituo Vya Afya Katika Vyuo Vikuu

Portrait of smiling african student walking by stairs with bag and smart phone
Baraza la Mawaziri jana Jumanne liliidhinisha uzinduzi wa vituo vya elimu bora na mafunzo ya afya vinavyolenga kuboresha huduma za saratani nchini Kenya.
Hatua hii ni pamoja na ile ya wahudumu wa afya kati ya Kenya na Uingereza chini ya mfumo wa Kenya UK Health Alliance (KUKHA).
Katika mkutano ulioongozwa na Rais William Ruto, Jumanne katika Ikulu ya Nairobi, Baraza la Mawaziri lilibaini kuwa matibabu na utafiti wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (NCD’s), Magonjwa ya Kupumua, , Malaria, ukimwi, Afya ya Akili, na Matibabu ya Saratani yatolewa kupitia vyuo vikuu.
Kama hatua ya kwanza kuelekea kufanikisha hatua hizo ambazo zinaahidi kupata huduma bora za afya ya juu katika maeneo ya Ziwa Magharibi na Mikoa ya Ufa Kusini mwa Kenya, Baraza la Mawaziri liliona kwamba matibabu na utafiti wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (NCDs), yataanza kuhudumiwa katika vyuo kama vile: Chuo Kikuu cha Kisii, cha Egerton, cha Maseno, Chuo Kikuu cha Masinde Muliro, Chuo cha Kibabii, na Chuo Kikuu cha Bomet.
Kadhalika Usimamizi wa Chuo Kikuu cha Egerton katika kaunti Nakuru umeanza mikakati ya kuwapiga kalamu baadhi ya wafanyakazi pamoja na kufutilia mbali kozi nane ambazo hazijafikisha idadi ya wanafunzi zaidi ya kumi na watano ili kupunguza gharama chuoni humo