EACC Kuchunguza Utajiri Wa Aliyekuwa Wa Usalama Wa Ndani Matiangi
Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imemwandikia Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, ikitaka nakala zilizoidhinishwa za mali ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i.
Kulinganana na Mkurugenzi Mkuu wa EACC, Twalib Mbarak, anamchunguza waziri huyo wa zamani na atatumia data hiyo kama ushahidi.
Kupitia barua iliyoandikwa Jumatatu, Februari 27, na kutiwa saini na Mbarak, EACC ilisema kwamba imeongeza uchunguzi wake na ingependa kuomba nakala zilizoidhinishwa pamoja na stakabadhi kutoka idara mbalimbali kutathmini jinsia Matiang’i alivyopata mali hizo.
Haya yanajiri siku chache baada ya idara Upelelezi na makosa ya jinai DCI, kumwita waziri huyo katika makao makuu yake ili kutoa mwanga kuhusu uvamizi unaodaiwa kufanywa na polisi katika makazi yake ya Karen wito ambao Matiang’i alipuuza.