Home » Wazazi Waibua Wasiwasi Juu Ya Hatua Ya Serikali Ya Kukata Ufadhili Kwa Wanafunzi Wa C+

Wazazi Waibua Wasiwasi Juu Ya Hatua Ya Serikali Ya Kukata Ufadhili Kwa Wanafunzi Wa C+

Wazazi wameibua wasiwasi kuhusu hatima ya wanafunzi huku serikali ikifikiria kupunguza ufadhili wa wanafunzi waliopata alama ya C+ katika mtihani wa kidato cha nne (KCSE).

 

Wakizungumza na wanahabari, baadhi ya wazazi wamelalamika kwamba hatua hiyo itawafungia nje maelfu ya watoto kutoka katika jamii duni kuendeleza masomo yao.

 

Joyce Kemunto ameeleza kuwa kuondolewa kwa usaidizi huo kutamaanisha kuwa mtoto wake ambaye alirudia kidato cha nne ili afuzu kupata ufadhili huo ataacha shule.

 

Mwanawe, Fred Sing’a, alipata alama ya C plain katika mtihani wa KCSE wa 2021 na akapelekwa katika shule ya ufundi stadi lakini akapoteza nafasi hiyo kwa sababu hakuweza kumudu kulipa karo yake.

 

Sing’a amedokeza kuwa iwapo serikali itatekeleza mpango huo, atafikiria kurudia tena ili afuzu kwa udhamini huo.

 

Mzazi wa pili amepinga hatua hiyo na kuionya serikali dhidi ya kubadili hitaji la msingi kuwa hifadhi ya matajiri katika jamii.

 

Iwapo serikali itaendelea na mpango huo, wanafunzi 70,088 watalazimika kuacha masomo ili kusaka fedha na kuendelea na masomo yao.

 

Taarifa hiyo imetolewa na afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Chuo Kikuu Geoffrey Monari ambaye amedokeza kuwa hazina haina uwezo wa kufadhili wanafunzi wote elfu mia 173,345 waliohitimu kujiunga na chuo kikuu.

 

Monari amedai kuwa upangaji huo utatokana na upatikanaji wa fedha na utaendeshwa na Huduma ya Vyuo Vikuu vya Kenya (K.U.C.C.P.S).
Hisia zake zinajiri baada ya Afisa Mkuu Mtendaji wa K.U.C.C.P.S Dkt Agnes Wahome kutoa wito kwa vyuo vikuu kuzingatia vyanzo vingine vya ufadhili wa wanafunzi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!