Home » Mwanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Bomet Adaiwa Kumdunga Kisu Mpenziwe Baada Ya Kuachana

Mwanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Bomet Adaiwa Kumdunga Kisu Mpenziwe Baada Ya Kuachana

Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Bomet amemdunga kisu mpenziwe kifuani baada ya kumwambia kuwa mapenzi yao yameisha na walipaswa kuachana mara moja.

 

Kulingana na naibu kamanda wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Bomet ya Kati Bashir Ali, kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa amemtembelea mpenzi wake katika eneo la makazi yake viungani mwa mji wa Bomet akiwa na rafiki mwingine wa kike.

 

Mpenzi wake, 25, ambaye pia ni mwaka wa tatu katika chuo hicho, alichukua jukumu la kumueelezea kijana huyo kuhusu kusitisha uhusiano wao ambapo vurugu zimeshuhudiwa na kuelekea katika kifo chake.

 

Kijana huyo anadaiwa kupandwa na gadhabu na kutoa kisu alichokuwa amekificha kwenye nguo yake ya ndani na kumchoma kifuani, ambapo alianguka chini mara moja na kufariki papo hapo.

 

Rafikiye wa kike ambaye alikuwa pamoja naye alimzuia asifanye madhara zaidi na kupiga kelele, ambapo alivutia hisia za wakazi ambao waliofika na kushuhudia tukio hilo.

 

Mshukiwa huyo amekamatwa na maafisa wa usalama na kufikishwa katika kituo cha polisi cha Bomet central kwa mahojiano.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!