Home » Mahakama Yasitisha Wito Wa DCI Kwa Wakili Danstan Omari

Mahakama kuu imetoa maagizo ya kusitisha kufikishwa kwa Wakili Danstan Omari mbele ya idara ya upelelezi na makosa ya jinai DCI ili kuhojiwa kuhusu shambulio la polisi katika nyumba ya aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiangi.

 

Jaji Jairus Ngaah ametoa maagizo hayo kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi hiyo baada ya Omari kuwasilisha ombi la kupinga uamuzi wa DCI wa kumwita.

 

Aidha, Ngaah amemtaka Omari kuwasilisha ombi la msingi ndani ya siku saba ambalo litawasilishwa kwa DCI.

 

Omari alikuwa amefika mahakamani akitaka kuzuia DCI kumwita akiteta kuwa wito huo ulitolewa bila msingi wowote wa kisheria na ulilenga kumtisha asiwakilishe mteja wake.

 

Wakizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya uamuzi huo, mawakili wa chama cha mawakili LSK wamesema wito uliotolewa na DCI kwa Danstan Omari ni shambulio dhidi ya mawakili nchini.

 

Kesi hiyo itatajwa Machi 8 kwa maelekezo zaidi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!