Home » Kamera Za CCTV Kuwekwa hospitali Za Kiambu

Gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi ameanza mikakati ya kuimarisha huduma za afya na kudhibiti ufisadi huku kukiwa na wasiwasi na pingamizi kutoka kwa wakazi.

 

Hatua hizo ni pamoja na kutundikwa kwa kamera za CCTV katika vituo vyote vya afya vya umma ili kuzuia utoroshwaji wa dawa na vifaa vya matibabu.

 

Hii itajumuisha hospitali zote za Level 5, Level 4 na Level 3 kati yao Thika, Kiambu, Gatundu, Kihara, Ruiru, Lari, Igegania, Githunguri, Tigoni, Wangige, Karatu, Karuri, Lusigetti, Kigumo, Githurai, Langata, Gachororo, Nyathuna, Ngoliba na Kiandu.

 

Kamera zitarekodi matukio yote kwenye viingilio, njia za kutoka, lifti, ngazi, maduka ya dawa,, maeneo ya kusubiri na ya mbele, pamoja na trafiki ya wagonjwa, wafanyakazi wa matibabu na wageni.

 

Marekebisho hayo yanakuja huku Wamatangi akifichua jinsi mashirika ya kibiashara yamekuwa yakipora hospitali za mitaa na za umma.
Kwa mfano, katika hospitali ya Kihara Level 4, mashine ya maabara ya Shilingi milioni 10 iliharibiwa na haiwezi kutumika tena.

 

Haya yanajiri huku Mbunge wa Thika Mjini Alice Ng’ang’a wiki jana akikashifu hali ya kusikitisha ya vituo vya afya katika kaunti hiyo, haswa hospitali ya Thika Level 5, na kumpa Wamatangi wiki moja kusafisha uchafu huo la sivyo waandamane.

 

Vile vile, Mbunge wa Kabete Githua Wamacukuri kando na hayo alimwambia Gavana Wamatangi kuchukua hatua madhubuti kuhusu sekta ya afya inayodorora.

 

Alisema miili ya wagonjwa waliofariki hukaa Hosptalini hadi siku mbili kabla ya kuondolewa.

 

Wamatangi alisema anashirikiana na wafadhili wa kimataifa na Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF) katika uanzishaji unaoendelea wa mpango wa afya kwa wote UHC.

 

Akizungumza eneo la Ngecha, Kaunti Ndogo ya Limuru, alisema baada ya usajili wa watu wengi unaoendelea utakaokamilika Machi, data hiyo itaunganishwa na itasaidia kuweka angalau watu milioni moja katika mpango wa bima ya afya ya umma.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!