Home » Wanakandarasi 2 Wa Majani Chai Katika Ufichuzi Wa BBC Watimuliwa

Nuwara Eliya, Sri Lanka

Shinikizo limeendelea kuongezeka kwa serikali ya Kenya kufuatia kufichuliwa na BBC kuhusu unyanyasaji wa kijinsia kwenye mashamba ya chai huko Kericho.

 

Wabunge wawili wametaka hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya wahusika wa uhalifu unaotekelezwa dhidi ya wafanyakazi wa majani-chai wanawake, kama ilivyonaswa na kipande cha uchunguzi.

 

Akizungumza Bungeni Mwakilishi wa Wanawake wa Kericho Beatrice Kemei ameitaka Kamati ya Leba kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa.
Mbunge huyo ametaka kujua hatua zinazochukuliwa na serikali kulinda haki za wafanyakazi wa kike na kuhakikisha kuwa wahusika wanawajibishwa.

 

Kwa upande mwingine, Mbunge wa Dagoretti Kaskazini Beatrice Elachi amelaani unyanyasaji wa wanawake, akitaka hatua zichukuliwe.

 

Wakati huo huo, James Finla msimamizi wa kampuni ya Uingereza, imesitisha mkataba wake na watu wawili walioangaziwa katika uchunguzi wa BBC.

 

Kipindi cha BBC cha Africa Eye kilikuwa na taarifa za kushtua za unyanyasaji wa kingono kutoka kwa wanawake wanaofanya kazi katika makampuni ya chai baada ya mwandishi wake kutumia miezi 18 kuchunguza suala hilo.

 

Kampuni hiyo ilifichua kuwa ilikuwa imeanzisha uchunguzi huru kubaini kilichotokea na maeneo ya kuboresha.

 

Kulingana na Finlay’s, aliongeza kuwa amejitolea kikamilifu kuchukua hatua madhubuti juu ya matokeo ya uchunguzi ili kuzuia uzoefu kama huo katika siku zijazo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!