Home » Vikao Vya Kuchunguza Irene Masit Kuendelea Hii Leo

Jopokazi linalochunguza mwenendo wa Kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC aliyesimamishwa kazi Irene Masit litaendelea na kikao chake leo hii Jumatatu.

 

Usimamizi wa jopo hilo uliahirisha kikao hicho kutoka Februari 9 hadi februari 20 saa 10 asubuhi.

 

Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika katika Taasisi ya Kenya ya Ukuzaji Mitaala jijini Nairobi.

 

Jopo hilo linaloongozwa na Jaji wa Mahakama ya Juu Aggrey Muchelule lilihitimisha kusikizwa kwa ushahidi wa mashahidi mnamo Januari 24 baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kutoa ushahidi wake.

 

Wakili wa Masit Donald Kipkorir alidokeza kuwa mteja wake hakutaka kuwasilisha shahidi yeyote
Mkuuhuyo wa zamani wa wakala wa uchaguzi alihojiwa kuhusu masuala yanayohusu mwenendo wa uchaguzi mkuu wa Agosti 9 hadi pale ombi lilipowasilishwa na kutupiliwa mbali na Mahakama ya Juu.

 

Masit ndiye kamishna pekee ambaye mwenendo wake wakati wa uchaguzi ulichunguzwa na jopo hilo baada ya wenzake watatu kujiuzulu.
Waliojiuluzu Walijumuisha aliyekuwa makamu mwenyekiti Juliana Cherera na makamishna Justus Nyang’aya na Francis Wanderi.
Mnamo Desemba 2, 2022, Rais William Ruto alimteua Muchelule kuwa mwenyekiti wa jopokazi hilo.

 

Pia aliwateua Carolyne Kamende Daudi, Linda Gakii Kiome, Mathew Njaramba Nyabena na Kanali Mstaafu Saeed Khamis Saeed kuwa mjumbe wa jopo hilo.

 

Kibet Kirui Emmanuel na Irene Tunta Nchoe waliteuliwa kuwa makatibu pamoja.

 

Wakili mkuu wa jopo hilo ni Peter Munge Murage ambaye anasaidiwa na Zamzam Abdi Abib.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!