Home » Rais Ruto Ahimiza Uwajibikaji Kwa Wachafuzi Wa Mazingira Duniani

Rais wa Kenya William Ruto ametoa wito kwa nchi tajiri kuwajibishwa kwa kuchochea ongezeko la joto duniani na kufanya marekebisho ya taasisi za fedha za kimataifa ili kukabiliana vyema na mabadiliko ya hali ya hewa.

 

Mataifa maskini, hasa yale barani Afrika, yameathiriwa vibaya na mabadiliko ya hali ya hewa, ambayo yamezidisha ukame na mafuriko, licha ya kuwajibika kiwango cha chini.

 

Katika mahojiano kando ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, ambapo mabadiliko ya hali ya hewa ni mada kuu, Ruto alisema wakati umefika wa “mabadiliko ya dhana”.

 

Kwa miaka mingi, serikali za Kiafrika zimekuwa zikitaka wachafuzi wakuu duniani walipe madhara ambayo uzalishaji wao umesababisha, unaojulikana kama “hasara na uharibifu”.

 

Duru ya hivi punde ya mazungumzo ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika nchini Misri mwaka jana yalikubaliana juu ya mfuko wa kufidia gharama ambazo nchi zinazoendelea zinakabiliana nazo kutokana na majanga ya asili yanayohusiana na hali ya hewa na athari kama vile kupanda kwa kina cha bahari.

 

Rais ruto alisema ni lazima bara la Afrika lichukuliwe kama mshirika mkuu na kwamba mfumo wa fedha duniani lazima ufanyiwe marekebisho iwapo matokeo yoyote yatapatikana.

 

Kulingana na Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema katika mkutano huo siku ya Jumamosi kwamba mataifa ya Afrika yanakabiliwa na mfumo wa fedha “usiofanya kazi na usio wa haki” ambao unawatoza viwango vya “unyang’anyi” wa riba.

 

Wanasayansi wanaonya kuwa ukame, mafuriko, dhoruba na mawimbi ya joto yatazidi kuwa na nguvu na mara kwa mara kutokana na ongezeko la joto duniani.

 

Pembe ya Afrika ni mojawapo ya maeneo yaliyo hatarini zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa, na matukio ya hali mbaya ya hewa yanatokea kwa kuongezeka kwa mzunguko na nguvu.

 

Nchini Ethiopia, Kenya na Somalia, karibu watu milioni 22 wako katika hatari ya njaa katika maeneo yaliyokumbwa na ukame mbaya zaidi katika miongo minne, kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa.

 

Miongoni mwa masuala mengine, viongozi wa Afrika wanakutana mjini Addis Ababa kushughulikia ukame uliorekodiwa na kuanzisha mkataba wa biashara huria unaoyumba katika bara la watu bilioni 1.4.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!