NCCK Yateuliwa Kwa tuzo La Nobel Kutokana na Juhudi Zake Za Kidemokrasia

Kamati ya Huduma ya Marekani na kundi la Quaker Peace & Social Witness imependekeza Baraza la Kitaifa la Makanisa ya Kenya (NCCK) na Muungano wa Urejesho wa Haki za Florida (FRRC) kwa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2023.
Uteuzi huo umetokana na msingi wa jukumu lao katika kukuza amani na haki za kidemokrasia wakati wa uchaguzi.
Ikumbukwe kwamba hapa nchini Kenya NCCK imetoa mchango mkubwa katika kuleta demokrasia nchini ,kurejesha siasa za vyama vingi, kurekebisha Katiba ya Kenya, uchunguzi wa uchaguzi, kujenga amani, kulinda haki za binadamu za raia na kukuza mazungumzo na upatanishi kwa miongo kadhaa.
Huu ni uteuzi wa kwanza wa shirika lenye msingi wa imani.
Shirika hilo limepongezwa kwa kazi yake ya kushughulikia vitisho vya kimataifa kwa serikali ya kidemokrasia na haki za kupiga kura.
Katika taarifa iliyoandikwa Februari 18, mwenyekiti wa NCCK Askofu Mkuu Timothy Ndambuki na katibu mkuu Rev Canon Chris Kinyanjui walishukuru Kamati ya huduma ya Marafiki wa Marekani na Quakers Peace and Social Witness kwa uteuzi huo.
Marehemu Prof Wangari Maathai alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka wa 2004 kwa mchango wake katika maendeleo endelevu, demokrasia na amani.