Home » Rais Ruto: Afrika Inafaa Kutengeneza Dawa Zake Yenyewe

Wakati umefika kwa Afrika kuanzisha na kudumisha taasisi imara za afya ya umma.

Rais William Ruto anasema bara la Afrika pia linafaa kuimarisha uwezo wake wa kutengeneza chanjo zake na kuacha kutegemea uagizaji wa bidhaa kutoka nje.

 

Akizungumza mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo Jumamosi, wakati wa kongamano la kwanza la mawaziri na Vituo vya Afrika vya Kudhibiti Magonjwa, Rais amesema Afrika lazima iwekeze katika nguvu kazi ya afya ya umma ili kusaidia taasisi zenye wataalamu wenye ujuzi.

 

Amebainisha kuwa harakati hizo zinahitaji kuongezeka kwa uwekezaji wa ndani katika afya na uhamasishaji thabiti wa rasilimali.

 

Rais amesema mabadiliko hayo ni muhimu kwa sababu vitisho vya kiafya vya siku zijazo na milipuko ya magonjwa “itakuwa ngumu zaidi na mbaya”.

 

Aidha amepongeza wito wa Tume ya Umoja wa Afrika kwa serikali, mashirika ya kimataifa na sekta ya kibinafsi kusaidia utekelezaji kamili wa Agizo la Afya ya Umma la Afrika.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!