Home » ‘Ajali Ya Ndege’ Tanzania

Asubuhi ya leo kuliripotiwa taarifa ya ajali ya ndege iliyotokea mita 150 kutoka katika uwanja wa ndege wa Kahama, mkoani Shinyanga nchini Tanzania na kusababisha vifo vya watu 10.

 

 

Taarifa ilielezea ajali hiyo ilihusisha ndege aina ya Garet 5Q KTM iliyokuwa na abiria 42 ikitokea Rwanda kuelekea Msumbiji kupitia Dar es Salaam.

 

 

Hata hivyo, ikiwa njiani ilipata hitilafu ikatakiwa kutua kwa dharura katika uwanja mdogo wa ndege wa Kahama ambapo kabla ya kutua ikaanguka na kupoteza maisha ya watu hao.

 

 

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita ameiambia BBC kuwa hakukuwa na ajali ya ndege isipokuwa ni zoezi la kawaida la utayari linalofanywa kila wakati na Mamlaka za ndege.

 

 

‘Tulipokea taarifa ya ajali tukaja mpaka eneo la ajali tukakuta sio ajali ni zoezi la utayari’ alisema Mhita na kuongeza ‘Hata sisi hatukujua ni zoezi linaloendeshwa kwa usiri ili kuona ni namna gani uwanja wetu na vyombo vyetu vyote vinawajibika ipasavyo yanapotokea matukio ya ajali’, alisema.

 

Awali kulionekana magari ya wagonjwa yakikimbiza majeruhi kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kahama ambapo hata baadhi ya watumishi katika Hospitali hiyo hawakuwa wanajua.

 

‘Mmoja wa watumishi aliyekuwa zamu ya usiku aliiambia BBC’ nimeambiwa magari ya wagonjwa yanapeleka majeruhi hospitalini’,

 

Amina Mbwambo mwandishi wa habari Kahama aliiambia BBC ‘ukiangalia ni kweli kama ajali maana ambulence(magari ya wagonjwa) ni nyingi mno na watu wanajifanya wamezimia wanaebbwa ila wakifikishwa Hospitali ndani ni wazima kabisa’, alisema.

 

 

Kwenye mitandao ya kijami baadhi ya watu walionyeshwa kusikitishwa na wengine kutoa pole wakidhani ni kweli ajali imetokea.

 

 

Zoezi hili la utayari linatokea ikiwa kumbukumbu ya ajali ya ndege ya Precision Air iliyoanguka katika ziwa Victoria na kuua watu 19 haijawatoka.

 

 

Ajali hiyo ilitokea Novemba 6, 2022 ikihusisha ndege ya PW 494 ilipokua inataka kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba (BKZ).

 

 

Mazoezi haya ya utayari hufanyika mara moja kila baada ya miaka miwili chini ya Mamlaka ya viwanja vya ndege.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!