Home » LGBTQ Inaongezeka Nandi –Naibu Gavana Mitei

Naibu Gavana wa Nandi Dkt.Yulita Mitei ana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja LGBTQ katika kaunti hiyo.

 

Kulingana na Mitei, ushoga na usagaji ambao unachukuliwa kuwa mwiko katika tamaduni ya Nandi unazidi kushika kasi katika kaunti hiyo akidai kwamba, utafiti wa hivi majuzi ulionyesha Nandi ina zaidi ya watu 1000 wanaojitambulisha kama LGBTQ.

Akizungumza katika taasisi ya Aldai Technical Mitei, amesema kuwa iwapo maovu hayo hayatashughulikiwa, yataonekana kama kawaida.
Ametoa wito kwa wazazi kuingilia kati na kuzungumza juu ya tabia hii mbaya, haswa kwa watoto wanaoenda shule.

 

Wasiwasi wake unakuja wakati makanisa ya Kianglikana nchini Kenya yamechukua msimamo dhidi ya ndoa za jinsia moja, yakihoji kuwa ni kinyume na mafundisho ya Biblia.

 

Kanisa linaloongozwa na Askofu Mkuu Ole Sapit, Jumapili lilipinga uamuzi wa Kanisa la Uingereza, ulioruhusu makasisi kuongoza ndoa za wapenzi wa jinsia moja inayojulikana na waumini wake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!