Home » Baadhi Ya Washirika Wa Azimio Kukumbana Na Shoka

Mbunge wa Kathiani Robert Mbui amedai kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mbunge mteule Sabina Chege baada ya kukutana na Rais William Ruto Ikulu pamoja na timu ya wabunge wa chama cha Jubilee.

 

Akiongea kwenye kipindi cha Runinga moja humu nchini, Mbunge Mbui amesema kuwa Sabina atang’olewa kutoka kwa wadhifa wa ubunge anaoshikilia kama Naibu Kinara wa Wachache, akidai hatakuwa na ufanisi tena katika kuwawakilisha wachache.

 

Haya yanajiri baada ya Sabina na baadhi ya wabunge wa Jubilee kufanya mkutano na Rais Ruto jambo ambalo limezua mvutano ndani ya chama na muungano wa Azimio la Umoja.

 

Wabunge hao pia wamejitolea kufanya kazi na serikali ya Ruto katika kufanikisha ajenda ya Kenya Kwanza.

 

Mbunge Mbui pia ametoa maoni yake kuwa upo uwezekano wa baadhi ya wabunge hao ‘kurejea’ kwenye muungano wa Azimio la Umoja akibainisha kuwa mazungumzo ya maendeleo ambayo yalitajwa kuwa ajenda za mikutano hiyo hayatatimia.

 

Amesema kuwa Hazina ilitangaza kuwa uchumi wa nchi uko katika hali mbaya na kwamba hakuna rasilimali za kufadhili matumizi muhimu ya umma.

 

Pia ametupilia mbali uwezekano wa wajumbe zaidi kukutana na Mkuu wa Nchi, akithibitisha kuwa wanachama waliosalia wameahidi kikamilifu uaminifu kwa muungano wa Azimio.

 

Aidha, kumekuwa na mvutano ndani ya chama cha ODM baada ya baadhi ya wanachama wake kukutana na Rais Ruto na kinara wa chama hicho Raila Odinga amewataja kama wasaliti na kwamba wanapaswa kujiuzulu kutoka kwa chama hicho.

 

Wabunge wa ODM wanaokabiliwa na shoka ni Gideon Ochanda (Bondo), Elisha Odhiambo (Gem), Mark Nyamita (Uriri) na Caroli Omondi (Suba Kusini), Paul Abuor (Rongo), Felix Odiwuor almaarufu Jalang’o (Lang’ata) na Seneta wa Kisumu Tom Ojienda.

 

Kwenye kundi la Jubliee kuna Mbunge wa Eldas Aden Keynan, John Waluke (Sirisia), Mark Mwenje (Embakasi Magharibi), Sabina Chege (Aliyependekezwa), Stanley Muthama (Lamu Magharibi) na Yusuf Hassan (Kamukunji) miongoni mwa wengine.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!