Home » Kesi Ya Ulaghai Ya Milioni 159 Dhidi Ya Aliyekuwa MD Ken Tarus Yaondolewa

Kesi Ya Ulaghai Ya Milioni 159 Dhidi Ya Aliyekuwa MD Ken Tarus Yaondolewa

Mahakama ya kupambana na ufisadi nchini Kenya imemruhusu Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ODPP kufuatilia kesi inayomkabili aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Kenya Power, Dkt Ken Tarus kutokana na ukosefu wa ushahidi unaomhusisha na kesi hiyo.

 

Wakati akiachilia Tarus, hakimu wa mahakama Elizabeth Juma amesema kuwa mahakama haiwezi kuendelea na kesi hiyo au kulazimisha ODPP kufanya hivyo.

 

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji, ameeleza kuwa ataendelea na kesi dhidi ya maafisa wengine wanane wanaodaiwa kutoa kandarasi kwa kampuni zilizosababisha malipo ya ulaghai ya shilingi milioni mia 159.

 

Pamoja na Tarus, watu wengine wanane waliokuwa wameshtakiwa, akiwemo meneja mkuu wa mitandao Daniel Tare, meneja mkuu wa ugavi Daniel Muga, na meneja wa zamani wa fedha Harun Karisa.

 

Wengine walikuwa wanakamati ya zabuni Benard Muturi, Evelyne Amondi, Noah Omondi, John Njehia na James Muriuki.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!